Occupational Safety and Health Authority
  +255-22-2760548 / 2760552       info@osha.go.tz                     

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

  • UJUMBE WA MTENDAJI MKUU

fsdfsd
Khadija Mwenda
Mtendaji Mkuu

Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) ni chombo cha kusimamia usalama na afya mahala pa kazi kwa kuhakikisha kwamba waajiri wote nchini wanaweka miundo na mifumo inayohakikisha usalama na afya mahala pa kazi vinalindwa.  

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la idadi ya waajiri wanaotuma maombi kuomba kukaguliwa au mafunzo ya usalama na afya makazini mwao. Hiki ni kiashiria muhimu cha mafanikio. Taasisi ya OSHA inatia mkazo katika kuelimisha kuliko kuadhibu ili kuhakikisha kwamba waajiri wanawajibika bila shurti.  

Hata hivyo, bado tunakabiliwa na changamoto kuu mbili; i) uelewa mdogo miongoni mwa waajiri na wafanyak Some Zaidi


DIRA

  • Kujenga nguvukazi salama na yenye afya njema kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu

DHIMA

  • Kusimamia, Kuwezesha, Kuelimisha na Kuhamasisha masuala ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwa kuweka mifumo thabiti itakayo zuia ajali, magonjwa na vifo pamoja na uharibifu wa mali ili kupunguza gharama za uendeshaji na kukuza uchumi wa Taifa.


Tunu Zetu

Image

Uadilifu

Wafanyakazi wa OSHA wakiwa sehemu ya watumishi wa umma wanapaswa kudhihirisha kiwango cha juu cha uaminifu, usawa na kuepuka upendeleo wa aina yoyote katika kuwahudumia wateja wetu wote kwa kiwango ambacho wateja watakuwa na imani na huduma zitolewazo.

Image

Huduma bora kwa wateja

Wafanyakazi wa OSHA wanapaswa kuonesha kiwango cha juu cha heshima, unyenyekevu na kujali muda katika kutekeleza majukumu yao ili wateja wanaopatiwa huduma waweze kuondoka wakiwa wameridhishwa zaidi ya matarajio waliyokuwa nayo.

Image

Uwazi

Wafanyakazi wa OSHA wanawajibika kuwa wawazi, makini na wepese katika kuwashirikisha wadau wetu taarifa mbali mbali.

Image

Uwajibikaji

Watumishi wa OSHA watawajibika kutokana na matendo yao na hivyo wanapaswa kuwa waaminifu katika utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kuzingatia  matumizi sahihi ya rasilimali za umma.

Image

Umahiri,nidhamu na ushikiano

Wafanyakazi wa OSHA wanawajibika kujitoa kwa kiwango juu kabisa na kufanya kazi kwa ushirikiano miongoni mwao katika jitihada za kufikia kiwango cha juu cha ufanisi pamoja na kuendelea kutafuta fursa za kuboresha zaidi viwango hivyo kupitia weledi uliopo na mafunzo endelevu.

Takwimu za Mwaka wa Fedha 2020/2021


Image

00

Maeneo ya Kazi Yaliyosajiliwa

Image

00

Maeneo ya kazi yaliyokaguliwa

Image

00

Wafanyakazi waliochunguzwa afya

Image

00

Watu waliopata mafunzo

Mahitaji ya Leseni ya kufuata (OSHA Compliance)

compliance

Sajili eneo lako la kazi na kupatiwa cheti cha usajili

compliance

Fanya tathmini ya hatari za usalama na afya katika eneo lako la kazi walau mara moja kwa mwaka

compliance

Andaa sera ya Usalama na Afya katika eneo la kazi husika

compliance

Hakikisha kwamba eneo lako la kazi limefanyiwa ukaguzi wa usalama na afya na wakaguzi stahiki kwa mujibu wa Sheria ya Afya na Usalama ya mwaka 2003

compliance

Hakikisha kwamba wafanyakazi wako wamefanyiwa uchunguzi wa afya zao kulingana na majukumu yao

compliance

Hakikisha kwamba wafanyakazi wanapatiwa mafunzo ya Huduma ya Kwanza, Kamati za Afya Usalama pamoja na mafunzo mengine muhimu